Kunauwezekano klabu ya Yanga ikamrejesha mchezaji wake mkongwe Kelvin Yondani.Mchezaji huyo aliachwa pamoja na beki wa kulia Juma Abdul ambao kwa nyakati tofauti ndani ya Yanga waliwahi kuvaa kitambaa cha unahodha.
Sababu ya kuachwa ni kushindwa kuelewana kwenye masuala ya kimkataba jambo lililofanya pande zote mbili kukubaliana kila mmoja aendelee na maisha yake.
Abdul mpaka anaachwa na Yanga baada ya mkataba wake kuisha alikuwa ni nahodha msaidizi.
Habari zinaeleza kuwa kwa sasa mabosi wa Yanga wameanza kufanya mazungumzo na Yondani ili kumrejesha ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kuendelea kupambana kwa msimu wa 2020/21.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli hivi karibuni alisema kuwa timu ipo imara kwenye usajili na ikiwa itahitaji saini ya nyota yoyote yule ni rahisi kumpata kwa kuwa wanajiamini.
"Mchezaji ambaye tutakuwa na malengo naye ni rahisi kwetu kumpata kwa kuwa uwezo tunao na tunatambua kwamba malengo yetu yapo kwenye jambo gani, bado tunaendelea na usajili hivyo wachezaji wetu wote tutawatambulisha Agosti 30 Uwanja wa Mkapa,".
0 Comments