VITA MPYA NDANI YA YANGA NANI ATAIMALIZA?


Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga amesema, GSM watakamilisha michakato yote ya usajili kama ilivyopangwa.Jana Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla aliwataka wanachama na wadau wote wa Yanga wachangie usajili wa nyota wawili wa kigeni

Aidha Dk Msolla akafafanua kauli hiyo kuwa alimaanisha wachezaji wapya nje ya hawa ambao tayari michakao yao ya usajili imekamilika.Injinia Hersi amesema wameisikia kauli ya Mwenyekiti lakini wanaamini ni maoni yake, kwani kwa upande wao wamejipanga kukamilisha michakato yote ya usajili

Hersi amewataka Wanayanga siku ya kesho Jumanne, wajitokeze kwa wingi uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wampokee kiungo kutoka Angola, Carlinhos
Aidha kuhusu ujio wa kocha, Mhandisi Hersi amesema Kaze ataondoka nchini Canada siku ya keshokutwa Jumatano, atatua nchini siku ya Ijumaa

"Nimeisikia kauli ya Mwenyekiti, labda ni mawazo yake lakini nawahakikishieni sisi GSM tupo imara kabisa kumalizia usajili tulioupanga"
"Kesho nawakaribisha Uwanja wa kimataifa wa JK kumpokea kiungo bora zaidi kushuka katika ardhi ya Tanzania"
"Kuhusu Mwalimu Kaze anatua siku ya Ijumaa akitokea Canada, ambapo ataondoka Canada keshokutwa Jumatano," amesema

Post a Comment

0 Comments