Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya Burundi Aigle Noir ndio watakaokuja kuipima Yanga siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi, Jumapili August 30 katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Mkapa
Akizungumza na Wanahabari mapema leo, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema klabu hiyo imethibitisha kuwa watakuja nchini kwa ajili ya mchezo huo.Yanga imefikia uamuzi wa kuwaleta Aigle Noir baada ya kupata changamoto ya kuzipata timu walizozihitaji mwanzo kutokana na nchi nyingi kuwa kwenye lockdown iliyosababishwa na corona
Aigle Noir walikuwa mabingwa wa Burundi msimu wa 2018-19, msimu uliopita wakimaliza kwenye nafasi ya tatu
0 Comments