BIASHARA YASHUSHA MASHINE MBILI ZA KIGANDA


Klabu ya Biashara United ya mkoani Mara imedhamiria kujiimarisha na kufanya vyema. Klabu hiyo kuelekea msimu wa 2020/21. Klabu hiyo imemasa Cleo Ssetuba na Joseph  Zziwa wachezaji kutoka nchini Uganda.

Wachezaji hao wamesajiliwa kama wachezaji huru na wataituikia klabu hiyo kwa miaka miwili.Ssetubba alikuwa mchezaji baada ya klabu yake ya Sony Sugar kuvunja mikataba na wachezaji wa klabu hiyo baada ya kushindwa kufanya vyema kwenye ligi kuu ,kufulisika na kushuka ligi kuu Kenya.

Kwa Upande wa Zziwa yeye alikuwa anaichezea Express FC lakini aliachana na klabu hiyo baada ya mkataba wake na klabu hiyo kumalizika na aligoma kuongeza.

Kocha mkuu wa Biashara United Francis Baraza amenukuliwa akisema "Tunataka timu imara kwa msimu wa 2020/21 . Tumefanikiwa kuwanasa wachezaji wawili wazuri tena wakiwa hawana timu.hiyo ni bahati ya kipekee kuwapata wachezaji wazuri kama hawa wakiwa hawana timu"Post a Comment

0 Comments