BARCELONA WATUMIA DAKIKA 45 KUIANGAMIZA NAPOLI


Klabu ya Barelona imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali baaada ya kuibuka a ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo mgumu dhidi ya Napoli. Ushindi huo umeifanya Barcelona kujikusanyia mabao 4-2 dhidi ya Napoli kwenye michezo miwili waliyokutana .

Unaweza kusema mchezo huo ulitumia dakika 45 tu kumalizana kwa timu hizo kwani mabao yote manne yalifungwa ndani ya dakika hizo. Clement Lenglet kutoka Barcelona ndiye aliyefungua lango la Napoli kwa kufunga bao murua dakika ya 10 tu kwenye mchezo huo. Lionel Messi aliongeza bao la pili dakika ya 23 huku Luis Suarez akifunga bao la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 45+1. Lorenzo Insigne aliipa Napoli bao la kufutia machozi dakika ya 45+5 kwa mkwaju wa penati. Timu hizo zilikwenda mapumziko Barcelona wakiongoza kwa mabao 3-1 .

Kipindi cha pili timu hizo zilicheza mpira wa kiwango cha juu huku Napoli wakijaribu kupiga mashuti mengi yasiyo na madhara langoni mwa Barcelona.

Bayern Munich inakwenda kukutana na Bayern Munich hatua ya robo fainali mchezo utakaopigwa ijumaa ya tarehe 14 Agosti 

Post a Comment

0 Comments