Klabu ya Barcelona imetangaza kuachana na mkurugenzi wa michezo klabuni hapo Eric Abidal. Mkurugenzi huyo amepigwa chini baada ya kura za maoni zilizopigwa na bodi kufuatia kipigo cha mabao 8-2 walichokipokea kutoka kwa Bayern Munich kwenye mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa ulaya.
Klabu hiyo imetangaza rasmi kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii kwa kuandika "Uongozi wa Barcelona na Eric Abidal umefikia makubaliano ya kusitisha mkataba kwa pande zote mbili, Klabu inatoashukrani kwa uadilifu.Kujitolea kwake pamoja na huduma mbalimbali ndani ya familia ya Barcelona.Tunamtakia bahati njema na mafanikio huko aendako
Abidal anakuwa mtu wa pili kufutwa kazi na Barcelona baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Quique Setien kuondoshwa mara baada ya kufungwa mabao 8-2 na Bayern Munich
0 Comments