AZAM FESTIVAL YAJIPANGA KUIFUNIKA SIMBA DAY LEO


Klabu ya Azam fc inahitimisha kilele cha wiki yake kwa shughuli kubwa itakayofanyika dimba la Azam Complex jijini Dar es salaam.

Hapo jana klabu ya Simba ilihitimisha wiki yao kwa siku maalumu ya Simba day huku tukishuhudia sapraizi kibao ikiwemo Diamond Platinumz aliyeshuka kwa ndege,Utambulishi wa wachezaji wapya wa timu hiyo na ushindi mkubwa wa mabao 6-0 

 Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu Arstica Cioaba raia wa Romania ina jambo lao ambalo litakuwa na burudani za kutosha kwa mashabiki wao.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin amesema kuwa:" Kwanza tunawaomba watu waje kwa wingi, kutakuwa na jogging, mechi ya timu zetu za vijana, timu yetu itacheza dhidi ya Namungo na msanii maarufu nchini King Kiba naye atakuwepo," amesema.

Ofisa Habati wa Azam FC, Thabith Zakaria amesema kuwa:"Mpira ni wa mashabiki na sio wa klabu, tunaenda kuwatambulisha wachezaji wao kwa ajili ya msimu ujao," amesema.

Pia, Msaga Sumu, naye atakuwepo kwenye Tamasha la Azam FC Festival ndani ya Azam Complex.

Msaga Sumu mbali na kutoa burudani kwa mashabiki watakaojitokeza kwenye tamasha hilo, pia atatambukisha wimbo wake alioitungia Azam FC.

Post a Comment

0 Comments