advertise with us

ADVERTISE HERE

SIMBA,YANGA NA AZAM PELEKENI MILIONI 50 KWA LUSAJO MILANGO IKO WAZI


Aliyekuwa Mshambuliaji wa Namungo Relient Lusajo amewaaga rasmi mashabiki wa klabu ya Namungo. Lusajo alikuwa na msimu mzuri ndani ya Namungo akifunga mabao 12  ligi kuu  msimu wa 2019/20.

Ni siku chache zimepita tangu mchezaji mwenzake Bigirima Blaise alipowaaga mashabiki wa timu hiyo. Lusajo alikuwa anawindwa na Yanga kurithi mikoba ya Yikpe,Molinga na Tariq walioachwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa kocha wa Namungo Thiery Hitimana ni kuwa mchezaji huyo amekwisha maliza mkataba wake na klabu hiyo na sasa yupo huru.

Lusajo alisema " Cha kwanza napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uzima mpaka siku ya leo pili ningependa kutoa shukran zangu za dhati kwa  uongozi pamoja na wachezaji wa Namungo kwa ujumla kwa muda wote tulioishi pamoja.

"Ushirikiano mlionipa tangu kujiunga na timu Daraja la Kwanza mpaka hapa tulipofika,bila kusahau mashabiki wote wa Ruangwa waliokua wakitupa hamasa na support iliyotuwezesha kufikia malengo ya klabu. Nawatakia kila la kheri Mungu awabariki katika msimu ujao,

Taarifa zinasema mchezaji huyo anahitaji dau la milioni 50 ili aweze kusajiliwa klabu yeyote lakini pia anahitaji mshahara  unaoeleweka. Vilabu vya Simba,Yanga na Azam vilikuwa vikimpigia hesabu na sasa ni wakati wao kupambana

Post a Comment

0 Comments