ALIYEMLETA KONDEBOY ANASTAHILI ZAWADI PALE SIMBA


Ni nani aliyemleta Luis Miquissone "KONDE BOY" pale Simba? binafsi aliyemleta mchezaji huyu anastahili kupewa gari kama zawadi kwa maana uwezo anaouonyesha kiungo huyo si mchezo.Luis Miquissone  amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Miquissone ndiye mchezaji pekee aliyehusika kwenye mabao yote mawili ya Simba akifunga bao la kwanza na kutoa pasi ya bao kwa John Bocco.

Miquissone alinukuliwa akisema:"Ninafurahi kuona timu inapata matokeo na kupata ushindi jambo ambalo ninalifurahia.Mimi ni kiungo ila naona nabadilika na kuwa mshambuliaji ninafunga na kutengeneza nafasi kwani ni timu na kazi tunafanya kwa kushirikiana hilo ni jambo jema na furaha kwetu."
Hili linakuwa ni taji la pili kwa Luis akiwa na Simba baada ya kuanza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara na leo la Shirikisho.
uis amefunga jumla ya mabao mawili ndani ya Kombe la Shirikisho, bao lake la kwanza aliwafunga Yanga kwenye mchezo wa nusu fainal uliopigwa Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo huo Simba ilishinda mabao 4-1.

Post a Comment

0 Comments