Habari zisizo rasmi zinasema kuna uwezekano kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Ibrahim Ajibu akaondoshwa klabuni hapo na kupelekwa kwa mkopo klabu ya KMC .Mwanzoni mwa msimu wa 2019/20 Ajibu alinunuliwa kutoka klabu ya Yanga na msimu uu ametoa pasi tano tu za mabao.
Msimu wa 2018/19 Ajibu alikuwa kila kitu ndani ya Ynga baada ya kuwa mfungaji bora kwa msimu huo pia akiongoza kutengeneza pasi 17 za mabao na kumfanya awe mchezaji bora wa Yanga kwa msimu huo.
Ndani ya Simba Ajibu amekuwa si kitu kuanzia kwa kocha Patrick Aussems mpaka Sven amekuwa akianzia benchi huku akizidiwa kila kitu na kiungo mzambia Clatous Chama aliyetengeneza nafasi 10 za mabao kwa timu hiyo.
Kama atakwenda KMC basi naamini atazidi kujiimarisha zaidi kwani ndani ya Simba kuna utitili wa viungo kuanzia Chama,Dilunga,Kahata,Shiboub,Miquissone ,Fraga,Mkude,Mlipili na hata yeye mwenyewe Ajibu
0 Comments