Klabu ya Yanga imefanikiwa kurejea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu iliyoshuka daraja Singida United. Paul Godfrey"Boxer' alikuwa wa kwanza kupa Yanga bao la kuongoza dakika ya 34 mchezo huo huku Mrisho Ngassa akifunga bao la pili dakika ya 38 .Steven Sey aliipa Singida bao la kufutia machozi dakika 45 ya mchezo.Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-1 . Mshambuliaji muivory coast Yikpe aliiandikia Yanga bao la tatu dakika ya 69 na kuifanya timu hiyo kujipatia pointi 3 muhimu.Yanga wamepanda kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 67 kwenye mechi 35 walizocheza msimu huu.Kipigo cha bao 1-0 walichokipata Azam dhidi ya Mtibwa Sugar kimeifanya timu hiyo kushuka mpaka nafas ya tatu wakiwa na pointi 65 kwenye michezo 35.
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments