Klabu ya Yanga imeshindwa kutamba mbele ya Biashara United ya mkoani Mara baada ya kulazimishwa sare ya kutofungana kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara. Biashara United imekuwa imara hasa inapokuwa dimba la nyumbani Matokeo haya yanaifanya Yanga kusalia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 61 nyuma ya Azam FC wenye pointi 62 huku timu zote zikicheza michezo 33. Kwa upande wa Biashara wao wamecheza michezo 33 wakiwa na pointi 45 huku wakishika nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi. Yanga inasafiri kuelekea mkoani Kagera kwa mechi nyingine ngumu dhidi ya Kagera Sugar mchezo wa ligi kuu utakaopigwa siku ya jumatano. Haya hapa matokeo mengine ya mechi
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments