Klabu ya Yanga imeitangazia vita Mwadui FC mchezo utakaopigwa leo jioni jijini Dar es salaam.Yanga imetangaza vita hiyo ikiwa na nia ya kujiimaisha nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara
Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa wamejipanga vema kushinda mbele
ya Mwadui FC ili wafikie malengo yao ya kumaliza ligi wakiwa nafasi ya pili.
“Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Mwadui, bado tuna malengo ya kumaliza ligi tukiwa nafasi ya pili hivyo ili tufikie malengo hayo ni lazima tushinde, mchezo wetu uliopita dhidi yao tulishinda hivyo itapendeza tukiwafunga tena,” amesema.
Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 inakutana na Mwadui FC inayopambana
kujinasua kushuka daraja ikiwa nafasi ya 17 na pointi 40 zote zikiwa zimecheza jumla ya
mechi 35.
0 Comments