ads

adds

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TAREHE 06-07-2020

Matumaini ya Chelsea ya kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Kai Havertz kutoka Bayer Leverkusen yameimarika baada ya mkurugenzi mtendaji wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge kusema kuwa klabu yake haiwezi kumlipa mchezaji huyo, 21 msimu huu. (Sun on Sunday)
Inter Milan imeanza mazungumzo na Chelsea ya kumnunua beki wa kushoto wa Italia Emerson Palmieri, 25, kutoka klabu ya Stamford Bridge. (Observer)
Willian and Pedro
Chelsea imeanza tena mazungumzo kuhusu makubaliano mapya na mshambuliaji wa Brazil Willian, ambaye amehusishwa na Arsenal na Tottenham baada ya mchezaji huyo, 31, kukataa ombi la kuhamia klabu ambayo haikutajwa huko China. (Goal)
Real Madrid inataka kumuuza mchezaji wa Colombia, James Rodriguez, 28, ambaye amesalia na mwaka mmoja kumaliza kandarasi yake badala ya kumpoteza mwaka ujao. Arsenal, Everton, Manchester United na Wolves inasemekana kwamba klabu zote hizo zimeonesha nia ya kutaka kumsajali. (Marca)
Jannik Vestergaard
Maelezo ya picha,
Leicester City itajitahidi kumsajili mlinzi wa Denmark Jannik Vestergaard kutoka Southampton, baada ya kumkosa mchezaji huyo, 27, mwezi Januari. (Goal)
Kocha wa Everton Carlo Ancelotti amesema kuwa kiungo wa kati wa Southampton, Pierre-Emile Hojbjerg alikuwa mchezaji mzuri lakini alikataa kujadili suala la uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo wa Denmark. (Liverpool Echo)
Southampton midfielder Pierre-Emile Hojbjerg
Hojbjerg pia analengwa na Tottenham, ambayo pia inataka kumsajili beki wa kulia wa Uingereza, 20, Max Aarons kutoka Norwich City. (Athletic, via Sunday Express)
Ancelotti ameongeza kusema kwamba hakuna vile beki ya kushoto wa Everton Lucas Digne ataruhusiwa kuondoka klabu hiyo msimu huu baada ya mchezaji huyo, 26, wa Ufaransa kuhusishwa na Chelsea na Manchester City. (Sunday Telegraph)
Mohammed Salisu
Maelezo ya picha,
West Ham imeungana na Everton, Manchester United na Southampton katika kuonesha nia ya kumwinda mlinzi wa Real Valladolid na Ghana Mohammed Salisu, 21. (Mail on Sunday)
Kocha wa Sunderland Phil Parkinson amesema hatma ya kiungo wa kati, 34, wa Jamhuri ya Ireland Aiden McGeady, ambaye yuko kwa mkopo Charlton, itaamuliwa mwisho wa msimu huu. (Sunderland Echo)

Post a Comment

0 Comments