advertise with us

ADVERTISE HERE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATANO TAREHE 22-07-2020


Juventus wanatafakari uwezekano wa kumnunua mkufunzi wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino kuchukua nafasi ya Maurizio Sarri kama kocha wao mpya. (La Stampa, via Mail)
Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 25. (Guardian)
Manchester United wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya £80m kwa Borussia Dortmund kumnunua winga wa England Jadon Sancho, 20. (Star)

Jadon Sancho

Maelezo ya picha,
Mkufunzi wa Rangers Steven Gerrard ndio chaguo la kwanza la Bristol City kuwa meneja wao mpya. (Bristol Post)
Chelsea wanazungumza na Bayer Leverkusen kuhusu mkataba wa £70m kumsajili Kai Havertz, baada ya klabu zote zilizokuwa zikimng'ang'ania kiungo huyo wa Ujerumani aliye na miaka 21 zikijiondoa katika kinyang'anyiro hicho. (Sky Sports)

Kai Havertz

Maelezo ya picha,
Chelsea watalazimika kumlipia kiungo wa kimataifa wa Slovenia Jan Oblak euro milioni 120 (£110m) ya kumruhusu kuhama ili kushinikiza mazungumzo ya ya uhamisho wa kipa huyo wa miaka 27- wa Atletico. (Goal)
Kiungo wa kati wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil, 31, amekataa ofa ya kujiunga na Fenerbahce inayoshiriki ligi kuu ya Uturuki . (Bild)

Mesut Ozil

Maelezo ya picha,echi zao
Lakini Ozil huenda akajiunga na ligi hiyo, Istanbul Basaksehir inasemekana iko tayari kumnunua. (90min)
Arsenal huenda wakaondoa masharti ya kulipa £40m katika mkataba wa mshambuliaji wa Sporting Joelson Fernandes ,17 katika kipindi cha saa 24 zijazo. (A Bola)
Licha ya dau lao kukataliwa, Tottenham wanamatumaini kuwa watakmilisha mchakato wa kumsajili beki wa Beijing Guoan na Korea Kusini Kim Min-jae, ambaye amepewa jina la 'Virgil van Dijk wa Korea Kusini'. (90min)

Kim Min-jae

Maelezo ya picha,
Newcastle wamekuwa wakimfuatilia kiungo wa kati wa Motherwell David Turnbull, 21,ambaye pia amehusishwa na Celtic. (Newcastle Chronicle)
Burnley wanamnyatia kiungo wa kati wa Southampton Harrison Reed, 25, ambaye mchezo wake Fulham umewavutia. (Football Insider)

Post a Comment

0 Comments