ads

adds

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAMOSI TAREHE 18-07-2020

Kocha wa Newcastle Steve Bruce anapanga uhamisho wa kiungo wa kati John McGinn, 25, raia wa Scotland ikiwa Aston Villa itashushwa daraja. (Star)
Leicester na Newcastle wameingia kwenye orodha ya timu zenye kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Norwich Todd Cantwell. (Mail)
Chelsea na Atletico Madrid zinafuatilia beki wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, 27, ambaye amehusishwa na kuhamia Manchester City. (Sun)
Hojbjerg
Kocha wa Southampton Ralph Hasenhuttl ameiambia Tottenham itoe ofa nzuri kwa kiungo wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 24, baada ya Everton kufungua uwanja wa kumwania mchezaji huyo kwa kitita cha karibu pauni milioni 25. (Evening Standard)
Kocha wa Tottenham Jose Mourinho anaamini kwamba kiungo wa kati wa Uingereza Oliver Skipp, 19, ambaye amesaini makubaliano mapya na klabu hiyo, ndio nahodha wa siku zijazo wa Spurs. Skipp anataka kuondoka kwa mkopo kupata ujuzi lakini Mourinho anapendelea mchezaji huyo asalie. (Evening Standard)
Tottenham iko tayari kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Wigan Alfie Devine, 15. (Mail)
Ferran Torres
Maelezo ya picha,
Manchester City imejitolea kwa kila namna kumsajili winga wa Valencia Ferran Torres, 20, lakini imeiarifu klabu ya Uhispania kwamba haitalipa zaidi ya euro milioni 35 sawa na (£31.8m) kwa mchezaji huyo. (Marca)
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema kwamba anataka kusalia na mshambuliaji Alexandre Lacazette, 29, katik klabu hiyo. (Evening Standard)
Aliyekuwa mlinda lango wa Uhispania Iker Casillas, 39, anarejea Real Madrid kama mshauri, miaka mitano baada ya kuondoka na kujiunga na Porto. (Marca)
Timothy Fosu-Mensah
Maelezo ya picha,
Manchester United itampa fursa mchezaji wa Uholanzi Timothy Fosu-Mensah, 22, ya kutafuta hatma yake ya kudumu katika klabu hiyo huku vilabu vingine vya Ujerumani vikijitokeza kuonesha nia ya kumwinda (Manchester Evening News)
Ikiwa Lacazette au mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, ataondoka msimu huu, Gunners huenda ikamlenga mshambuliaji wa Celtic raia wa Ufaransa Odsonne Edouard, 22. (Bleacher Report)
Arteta anasisitiza kwamba ombi lake la kuwekeza kwa kikosi chake mapema wiki hii, haikuwa jaribio la kutuma ujumbe kwa mmiliki wa Arsenal Stan Kroenke. (Express)
Quique Setien
Maelezo ya picha,
Kocha wa Barcelona Quique Setien anakubali kwamba hana uhakika ikiwa yeye ndiye atakayesimamia mechi ya pili ya Ligi ya mambingwa ya mechi 16 za mwisho dhidi ya Napoli. (AS)
Wakati huohuo, Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu ameitisha mazungumzo ya dharura na Setien. (ESPN)
Huku aliyekuwa kocha wa Ufaransa Laurent Blanc akipewa ofa na Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Post a Comment

0 Comments