advertise with us

ADVERTISE HERE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO IJUMAA TAREHE 10-07-2020


Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anatafakari uwezekano wa kumsajili beki wa kushoto wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28, msimu huu wa joto. (Mirror)
Ajenti wa Kevin de Bruyne anasema kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji mwenye aliye na umri wa miaka, 29, hataondoka Manchester City, msimu huu hata marufuku ya Ulaya dhidi ya klabu hiyo itaondolewa. (Sporza - in Dutch)
Arsenal inataka kusalia na kipa wa Argentina Emiliano Martinez, 27, baada ya kuahirisha mpango wa kumnunua kipa mpya msimu huu wa joto. (Mirror)
Emiliano Martinez
Real Madrid wako tayari kupokea ofa ya klabu zinataka kumnunua mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic, 22. (Marca)
Leicester City wanaamini watafanikiwa kumsajili Jovic kwa karibu £31m na kuthibitisha kuwa tayari wamewasiliana na ajenti wake. (Star)
Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc anasema klabu hiyo ya Ujerumani imetoa orodha ya wachezaji watakaojaza pengo litakaloachwa na na winga wa England Jadon Sancho, 20, endapo ataondoka msimu huo. (Kicker - in German)
Jadon Sancho
Maelezo ya picha,
Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameifahamisha klabu yake kwamba anataka kumsajili mshambuliaji atakayesaidiana na - Sancho ambaye wanamnyatia - pamoja na mshambuliaji wa wa safu ya kati na nyuma msimu huu. (Telegraph - subscription required)
Inter Milan inataka kuwasajili beki wa wa kushoto wa Italia Emerson Palmieri, 25, na mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, kutoka Chelsea. (Goal)
Olivier Giroud
Maelezo ya picha,
Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Roy Keane ameshindwa kuchagua ni nani anastahili kujiunga na klabu hiyo kati ya kipa wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris, 33, na mshambuliaji wa Korea Kisini Son Heung-min, 28. (Star)
Everton inakabiliwa na kibarua kigumu kumpata mlinzi wa Lille na Brazil Gabriel Magalhaes, 22,baada ya kuchelewa kuwasilisha ombi la kutaka kumnunu mchezaji huyo. (Sky Sports)

Post a Comment

0 Comments