advertise with us

ADVERTISE HERE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO IJUMAA TAREHE 03-07-2020


Chelsea na Manchester City wanaweza kugeuka kwenye mpango wa kumnasa beki wa kushoto wa Everton, Mfaransa Lucas Digne, 26, ikiwa itakuwa vigumu kumpata Ben Chilwell, 23, anayekipiga Leicester. (ESPN)
Everton, Liverpool, Manchester City na Manchester United wanatarajia kumshuhudia Leon Bailey, 22, siku ya Jumamosi, wakati ambapo winga huyo wa Bayer Liverkusen akiwa na matarajio ya kuhamia England. (Sky Sports)
Msenegali Kalidou Koulibaly ni miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na Pep gardiola kuimarisha safu yake ya ulinzi
Maelezo ya picha,
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amewaorodhesha wachezaji wa nafasi ya ulinzi ya Napoli, Msenegali Kalidou Koulibaly, 29, mchezaji wa Villarreal, Mhispania Pau Torres, 23, na mchezaji wa Benfica Mholanzi Ruben Dias ,23, akitarajia kufanyia mabadiliko safu yake ya ulinzi. (Times)
Sevilla wanajiandaa kufanya uhamisho wa mkopo wa mlinda mlango wa Chelsea Kepa Arrizabalaga, 25, ambaye mustakabali wake haujajulikana Stamford Bridge.
Valencia inamfuatilia kwa karibu mchezaji Eric Bailly wa nafasi ya ulinzi
Maelezo ya picha,
Manchaster United wako tayari kumruhusu Eric Bailly, 26 , kuondoka kwa mkopo msimu ujao wakati Valencia ikimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi. (Sun)
Mlinda mlango anayechezea Manchester United kwa mkopo Dean Henderson, 21, ameitahadharisha klabu kuwa hatasubiri milele kuwa chaguo lao la kwanza, kauli hii imekuja wakati Chelsea ikionesha nia na mchezaji huyo. (Express)
Dean Henderson, ameitahadharisha Manchester United kuwa hatasubiri milele kuwa chaguo lao la kwanza
Maelezo ya picha,
Chelsea inamfuatilia mlinda mlango wa Lille Mike Maignan, 24 na Alphonse Areola, 27 anayecheza kwa mkopo Real Madrid akitokea Paris St- Germain. (Express
Hatahivyo, Tottenham pia wanafikiria kumnyakua Magnan, huku kocha Jose Mourinho akimtolea macho mchezaji huyo kuwa mrithi wa mlinda mlango wa sasa Hugo Lloris, 33. (Sun)
Tim Sherwood anaamini nahodha Jack Grealish, 24, atajiunga na Manchester United msimu huu.
Maelezo ya picha,
Kocha wa zamani wa Aston Villa Tim Sherwood anaamini nahodha Jack Grealish, 24, atajiunga na Manchester United msimu huu. (Birminghma Mail)
imeweka mezani kitita cha pauni milioni 3.5 kwa ajili ya kiungo wa kati wa Reading John Swift, lakini Leeds pia wanamuhitaji mchezaji huyo. (Mail)
Jose Mourinho aapa kutomuachilia Giovani Lo Celso
Kocha mkuu wa Tottenham Jose Mourinho amesema hatambadilisha Giovani Lo Celso, 24 kwa Bruno Fernandes wa Manchester United, baada ya Spurs kumkosa kiungo huyo msimu uliopita. (Sky Sports)
Sheffield United wangependa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi Abdul Mumin, 22 kutoka FC Nordsjaelland msimu huu. (Mail)
Filip Kostic ,27, anaweza kuondoka Eintracht Frankfurt, huku InterMilan na klabu za rimia zikiwa zinamtolea macho winga huyo raia wa Serbia. (Goal )

Post a Comment

0 Comments