SIMBA WALISTAHILI UBINGWA VPL MSIMU HUU


Klabu ya Simba imetwaa rasmi ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kucheza michezo 34 na kupata pointi 81 huku wakiwa na faida ya mabao 53. Simba imetwaa ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo huku ikiweka rekodi mpya ya kutwaa ubingwa huo wakibakiwa na mechi 4 kumaliza ligi.

Klabu hiyo inayonolewa na mbelgiji Sven imefanya vizuri tangu mwanzo wa msimu ilipokuwa chini ya Patrick Ausems ambaye alitimuliwa raundi ya saba tangu ligi kuanza lakini kocha Sven alisimama imara na timu hiyo na kutwaa ubingwa huo.

Meddie Kagere anaongoza orodha ya wafungji bora akiwa  na mabao 19 huku Clatous Chama akiongoza orodha ya watengenezaji mabao akifanya hivyo mara 10 msimu huu.Aishi Manura anakuwa kipaaliyecheza mechi nyingi lakini amefungwa mabao machache zaidi.Swali linakuja ni nani ataibuka mchezaji bora wa msimu huu kwa klabu ya Simba na tuzo za bodi ya ligi.

Hizi ni baadhi ya picha wachezaji wa simba wakishangilia ubingwa wao 

Post a Comment

0 Comments