Sina uhakilka kama alibet mchezo huu wa Simba na Yanga na kama alifanya hivyo basi mwandishi mkongwe wa habari ,mchambuzi mahili wa masuala ya Kisiasa na mkurugenzi wa Karibu Tanzania Organization (KTO) Bw.Maggid Mjengwa basi atakuwa ameipatia fedha nyingi .
Maggid ndiye aliyeitabilia klabu ya Simba ushindi wa mabao manne dhidi ya Yanga na matokeo yamekwenda kama alivyosema kwani Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1.Gerson Fraga alifunga bao la kwanza dakika ya 21,Chama dakika ya 50 ,Miquissone dakika ya 52 na Mzamiru dakika ya 88 huku yanga wakipata bao la kufutia machozi kupitia Feisal Salum.
Maggid ni shabiki kindaki wa klabu hiyo yenye makao makuu mitaa ya Msimbazi Kariakoo na kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika ujumbe huu
" Mechi Nyingine za Simba Na Yanga wala haziumizi kichwa, kama ya leo...Kwamba Simba itashinda si swali.Mie najiuliza;
"Hivi leotutashinda kwa mangapi?" Yanga leo wana kazi sana ya kuchoma ubani yasisomeke mabao manne
Hii ni Screenshot ya ujumbe wa Maggid Mjengwa
0 Comments