BETI NASI UTAJIRIKE

SERIE A:JUVENTUS WAPIGWA COMEBACK YA HATARI ILIBAKI KIDOGO WAPIGWE


Klabu ya Juventus imeendelea kufanya vibaya ligi kuu Italy baada ya kuruhusu sare ya mabao 3-3 dhidi ya Sassuolo. Juventus wakiwa ugenini walianza kwa kupata bao la kuongoza dakika ya 6 tu kupitia beki wa kulia Danilo huku Gonzalo Higuan akishindilia bao la pili dakika ya 12 ya mchezo. 

Filip aliwarudisha mchezoni Sassuolo kwa bao maridhawa dakika ya 29 huku Berardi akiisawazishia Sassuolo bao la pili dakika ya 51 na Caputo akifunga bao la tatu dakika ya 54. 

Shukrani ziende kwa Alex Sandro alieisawazishia Juventus bao la tatu dakika ya 64 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 3-3. Mshambuliaji Cristiano Ronaldo aliambulia kadi ya njano kwenye mchezo huo.Kwa matokeo hayo Juventus inaendelea kuongoza Serie A wakiwa napointi 74 kwenye michezo 34 waliyocheza.

Hii inakuwa ni comeback ya tatu mfululizo baada ile ya kwanza na AC Milan walipotangulia kwa mabao 2-0 lakini mchezo ulimalizika kwa Juventus kufungwa mabao 4-2.huku mchezo dhidi ya Atlanta wakisawazisha dakika za nyongeza na mchezo huo kumalizika kwa sare ya 2-2.


Post a Comment

0 Comments