SERGIO RAMOS AZIDI KUDHIHIRISHA YEYE NI BEKI WA DUNIA REAL MADRID IKISHINDA


Beki kisiki wa Real Madrid Sergio Ramos ameendelea  kuwa mtetezi wa timu hiyo baada ya hapo jana kuipa bao la ushindi timu hiyo wa bao 1-0 kwenye mchezo wa La Liga dhidi ya Getafe.  

Ramos amekuwa mchezaji muhimu kwa Real Madrid msimu huu akicheza michezo 30 na kufunga mabao 8 akipiga jumla ya mashuti 30 huku 14 yakirenga golini. Msimu huu umekuwa mzuri kwa beki huyo mwenye miaka 34 kwani anakuwa mchezaji wa 2 ndani ya Real Madrid akiwa na mabao 8 huku anayeongoza ni Karim Benzema akiwa na mabao 14.

Ushindi wa Real Madrid dhidi ya Getafe unaifanya timu hiyo zidi kukaa kileleni kwa pointi 74 ikiipiku klabu ya Barcelona yenye pointi 70 kwenye michezo 33 waliyocheza 

Post a Comment

0 Comments