advertise with us

ADVERTISE HERE

SENZO: HAKUNA ATAKAYEONDOLEWA NDANI YA SIMBA


Mtendaji Mkuu wa klabu, Senzo Mbatha amekanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la Mwanaspoti kuwa tutafukuza benchi zima la ufundi kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21. Senzo amesema taarifa zilizochapishwa na gazeti hilo ni uzushi ambao unataka kuIchanganya klabu hiyo kuelekea mchezo wa fainali wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya Namungo, Agosti 2. Kiongozi huyo ameongeza kuwa hakuna mchezaji, kiongozi au mtu yoyote wa benchi la ufundi ambaye atafukuzwa kipindi hiki. "Nimesikitishwa na taarifa zilizotolewa na gazeti la Mwanaspoti ule ni uzushi mtupu hakuna mabadiliko yoyote yamefanywa kwenye benchi la ufundi. Niwatake Wahariri na maripota kuzifanyia uchunguzi taarifa zao kabla ya kuchapisha," amesema Senzo. Kuhusu usajili Senzo amesema watasubiri ripoti wa mwalimu baada ya kumalizika kwa msimu ili waone ni sehemu gani ya kufanya marekebisho. "Usajili bado tunasubiri ripoti ya mwalimu baada ya kumalizika kwa msimu. Kwa sasa tunaangalia mechi mbili za ligi zilizosalia pamoja na mchezo wa fainali," amesema Senzo.

Post a Comment

0 Comments