BETI NASI UTAJIRIKE

PIGO:NAMUNGO FC KUZIKOSA MASHINE ZAKE MBILI MUHIMU DHIDI YA SIMBA


Namungo FC kuwakosa wachezaji wake wawili muhimu kutokana na kusumbuliwa na majeraha.Leo itakuwa Uwanja wa Majaliwa dhidi ya Simba kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara. 

Thiery amesema kuwa, Relliants Lusajo ambaye ni nahodha wa kikosi hicho pamoja na Edward Manyama watakosa mchezo wa kesho dhidi ya Simba.

Lusajo ni mtupiaji namba moja ndani ya Namungo akiwa na mabao 12 na pasi zake tatu za mabao.Manyama anakumbukwa kwa kufunga mabao mawili mbele ya Yanga, Uwanja wa Taifa kwenye sare ya kufungana mabao 2-2.

Mchezo wao uliopita Uwanja wa Majaliwa, Namungo ilishinda bao 1-0  mbele ya JKT Tanzania huku Simba ikitoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Ndanda FC, Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Simba tayari ni mabingwa na kwenye mchezo huo watakabidhiwa Kombe lao la msimu wa 2019/20 baada ya mchezo.

Post a Comment

0 Comments