ads

adds

NINI KINAMKWAMISHA KAGERE ASIFUNGE KWA DAKIKA 208

Ligi Kuu Bara ilisimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona na Kagere alisepa zake Rwanda. Juni Mosi Serikali iliruhusu masuala ya michezo kuendelea.
Mpaka inatwaa ubingwa, Simba ilikuwa imecheza mechi tano ambazo ni sawa na dakika 360, huku Kagere akitumia dakika 208 na hajaambulia bao wala kutoa pasi ya bao kwenye mechi alizocheza.
Kwenye mechi dhidi ya Azam FC, alitumia dakika zote kukaa benchi akisoma mchezo na timu yake ilishinda mabao 2-0.
Alianza kucheza mbele ya Ruvu Shooting, Juni 14 aliyeyusha dakika zote 90 kwenye sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Taifa kisha mechi yake ya pili ikawa ni Juni 17 Uwanja wa Taifa dhidi ya Mwadui ambapo Simba ilishinda mabao 3-0, Kagere alitumia dakika 28.
Mwisho wa yote guu la kushoto la Kagere lilishindwa kufurukuta mbele ya Tanzania Prisons iliyo chini ya Kocha  Mkuu, Adolf Rishard Uwanja wa Sokoine ambapo aliyeyusha dakika zote 90 na kufanya atumie jumla ya  dakika 208 ndani ya uwanja bila kufurukuta.
Kagere anavutwa shati na mtupiaji namba moja wa Kagera Sugar, mzawa Yusuph Mhilu ambaye kibindoni ana jumla ya mabao 13.

Post a Comment

0 Comments