advertise with us

ADVERTISE HERE

NAPOLI WATUMA OMBI MAALUMU KUELEKEA MCHEZO NA BARCELONA


Klabu ya inayoshiriki Serie A nchini Italia  Napoli imetuma ombi maalumu kwa shirikisho la soka ulaya UEFA kuelekea mchezi wake wa marudiano ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Barcelona. Uongozi umetuma maombi ya mchezo huo unaopaswa kuchezwa dimba la Nou Camp nyumbani kwa Barcelona kuhamishwa na kuchezwa uwanja mwingine wowote nje ya nchi ya hispania kutokana na ongezeko kubwa la kuenea janga la Covid-19.

Raisi wa Napoli alinukuliwa akisema "Mchezo dhidi ya Barcelona ni mkubwa sana .Tulicheza na Barcelona kabla ya kuanza msimu na  tulicheza nao mara mbili kisha tukakutana hatua ya mtoano kwa raundi ya kwanza hatua ya 16 bora na huu mchezo wa marudiano utakuwa wa nne kukutana. 

"Tunaskia hofu imetawala hispania na hatujui UEFA watakuwa na mkakati gani kwani wao ndio wenye maamuzi

"Kama walisema michezo iliyobaki ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE itachezwa nchini Ureno huku ile ya EUROPA ikipigwa Ujerumani ,nafikiri michezo inayofuata ipigwe nchini Ujerumani au Ureno

"Sielewi kwanini mchezo huo upigwe kwenye mji wenye majanga zaidi

Itakumbukwa mchezo wa kwanza kati ya Barcelona na Napoli ulipigwa dimba la San Paolo Stadium uwanja wa nyumbani wa napoli na mchezo uliomalizika kwa klabu hizo kutoka sare ya mabao 1-1 magoli yaliyofungwa na Mertenes dakika ya 30 kabla ya Griezman  kusawazisha dakika ya 52.

Mchezo huo ni muhimu kwa klabu zote mbili kuelekea robo fainali ligi ya mabingwa Ulaya zitakazopigwa nchini Ureno 

Post a Comment

0 Comments