BETI NASI UTAJIRIKE

MWINYI ZAHERA ATAKA KURUDI YANGA AIKACHA SIMBA

Aliyewahi kuwa Kocha wa klabu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema amekasirishwa sana baada ya kusikia maneno aliyosema aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Luc Eymael. Zahera amesema ameshangaa kusikia kocha akilalamika kuwa hana DSTV amesema sio kila mzungu anayekuja Africa basi ni kocha mzuri. Zahera amesema Luc anavyolalamika kuwa halipwi vizuri anamshangaa maana huko kwao huwa hawapati hata shilingi elfu mbili.
Akihojiwa na Mtangazaji wa kituo cha redio alipoulizwa kuhusu ahadi aliyotoa ya kukatwa mkono au kulipa Dola elfu moja ambapo David Molinga ameshindwa kufikisha Magoli (15), Zahera amejibu ...
Nimefurahishwa sana kwa kile alichokifanya David Molinga Yanga walishindwa tu kumpa mechi kadhaa ndo maana hajafikisha magoli hayo (15), kuna mechi karibu (10) ambazo hakuchezeshwa bila sababu.
Na alipoulizwa Ikiwa klabu ya Yanga itakuhitaji tena awe kocha wake atakubali? Zahera akajibu.
Klabu ya Yanga iko moyoni mwangu (Naipenda) hatukuachana vibaya, ndio wakinihitaji ntakubali"
alipoulizwa kuhusu kama watamuhitaji Simba atakwenda ila kocha huyo aikataa kwa madai Simba wanakocha mzuri pia hivyo hawawezi kwenda
Kwanza hawawezi kuniita kwa sababu kocha aliyepo anafanya vizuri" 🔍 Mwinyi Zahera

Post a Comment

0 Comments