advertise with us

ADVERTISE HERE

MORRISON APANDA TENA JUU YA MPIRA,ATUMA SALAMU ZA VITISHO KWA SIMBA


Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Benard Morrison amerejea rasmi mazoezini na wachezaji wenzake wa Yanga na kwa mara nyingine ameupanda mpira kuonyesha ubora wake. Yanga hufanya mazoezi katika viwanja vya chuo cha Sheria na kwenye mazoezi hayo Morrison alionyesha kiwango kikubwa.

Mchezo wa ligi kuu katii ya Simba vs Yanga ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa kwa faulo iliyopigwa na Morrison. Kocha Eymael amethibitisha kuwa mchezaji huyo atakuwepo kwenye mechi nusu fainali julai 12 dhidi ya Simba 

Mara baada ya mazoezi Morrison alifunguka hatma yake ndani ya Yanga na alinukuliwa akisema 

Mimi ni mchezaji wa Yanga SC , Nna mkataba na Yanga SC labda wao ndo wanifukuze . . mengine ni changamoto tu za kazi naamini tutafikia suluhu nipo hapa kufanya kazi "

Picha za wachezaji wa Yanga mazoezini

Post a Comment

0 Comments