MORRISON AENDELEZA UBABE WAKE DHIDI YA KAGERA SUGAR


 Yanga SC wamewapa furaha mashabiki wao baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. 

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, winga ‘mtata’ kutoka Ghana, Bernard Morrison dakika ya 78 akimalizia pasi ya mchezaji mwenzake wa kigeni, mshambuliaji David Molinga Ndama ‘Falcao.

Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 64 baada ya kucheza mechi 34 na kubaki nafasi ya tatu, sasa ikizidiwa pointi 17 na mabingwa tayari, Simba SC kwa mara ya tatu mfululizo. 


Mechi nyingine za leo, KMC imeshinda 2-0 dhidi ya Singida United, mabao ya Charles Ilanfya dakika ya 39 na Mohamed Samatta dakika ya 85 Uwanja wa Azam Complex.
Na bao pekee la Waziri Junior dakika ya 64 likaipa Mbao FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.


Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara, wenyeji Biashara United wamelazimishwa sare ya 0-0 na Ruvu Shooting na Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Ndanda SC pia wametopa sare ya 0-0 na JKT Tanzania.


Kikosi cha Kagera Sugar kilikuwa; Benedict Tinocco, Mwata Gereza, David Charles, Juma Nyosso, Erick Bigirwa, Zawadi Mauya, Erick Mwaijage, Abdallah Seseme, Kelvin Sabato, Ally Ramadhan na Peter Mwalyanzi. 


Yanga SC; Farouk Shikaro, Deus Kaseke, Adeyoum Ahmed, Said Juma ‘Makapu’, Kelvin Yondan, Abdulaziz Makame/Yikpe Gislan dk55, Bernard Morrison, Feisal Salum, David Molinga/Lamile Moro dk86, Ditram Nchimbi/Patrick Sibomana dk55 na Erick Kabamba/Raphael Daudu dk46.


Post a Comment

0 Comments