MFUNGAJI BORA JAMIE VARDY AWEKA REKODI MPYA EPL


Jamie Vardy ameibuka mfungaji bora ligi kuu Uingereza msimu wa 2019/20 baada ya kufunga mabao 23 kwenye mechi 35 alizocheza. Vardy amewamwaga wafungaji kama Piere Aubemayang na Danny Ings wenye mabao 22 kila mmoja. 

Vardy anakuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kwa ligi kuu Uingereza kutwaa kiatu cha ufungaji bora akiwa na miaka 33.Mchezaji huyo amekuwa nguzo imara kwa Leicester city tangu ilipopanda daraja msimu wa 2015-16 akicheza michezo 286 na kufunga mabao 120 ndani ya klabu hiyo.

Leicester City imefunga mabao 67  na kuwa moja ya klabu zenye mabao mengi ikishika nafasi ya nne nyuma ya Chelsea mabao 69,Liverpool mabao 85 na Manchester City mabao 102. kati ya mabao 67 yaliyofungwa na klabu hiyo  mabao 23 yamefungwa na Vardy huku akisaidia upatikanaji wa mabao mengine manne.

Post a Comment

0 Comments