MECHI RIPOTI:AS ROMA YAICHAKAZA SPAL 6-1 SERIE A


Klabu ya As Roma imeendelea kusaka nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu Italy Serie A baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Spal. Mbao ya AS Roma yalifungwa na Kalinic dakika ya 10,Perez dakika ya 38,Kolarov dakika ya 47, Brono Peres dakika ya 52 na 75huku Nocolo Zaniola akifunga bao la sita dakika ya 90 ya mchezo huo. Alberto Cerri aliipa pal bao la kufutia machozi dakika ya 24.

Matokeo hayo yanaifanya Roma kufikisha pointi 61 kwenye michezo 35 iliyocheza huku ikiwa nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi.Klabu hiyo inapambana kupata nafasi ya 4 baada ya uachwa pointi 8 na Lazio walio nafasi ya 4 huku ikibakiwa na michezo mitatu. Swali ni je watatoboa 

Post a Comment

0 Comments