BETI NASI UTAJIRIKE

MECHI RIPOTI: SIMBA QUEENS YAICHAKAZA 6-0 MLANDIZI QUEENS



Timu ya Wanawake ya Simba Queens imeendelea kutoa dozi nene baada ya kuichakaza bila huruma Mlandizi Queens mabao 6-0 katika mchezo wa ligi uliopigwa uwanja Uhuru. Ushindi huu unatufanya kufika pointi 47 baada ya kucheza mechi 18 tukiendelea kubaki kileleni mwa msimamo huku tukisalia na michezo minne. Opa Clement ambaye yupo kwenye kiwango bora alitufungia bao la kwanza dakika ya 13 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 20.Nahodha Mwanahamis Omary 'Gaucho' ulitupatia bao la tatu dakika ya 39 na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili tulirejea kwa kasi kwa kuendelea kulisakama lango la Mlandizi na kufanikiwa kupata mabao mengine matatu yaliyofungwa na Asha Jafar, Doto Evarist na Jacky Albert 82. Baada ya mchezo wa leo kikosi kitashuka tena dimbani wikiendi hii kuikabili Tanzanite mtanange utakaopigwa uwanja huu huu wa Uhuru.

Post a Comment

0 Comments