advertise with us

ADVERTISE HERE

MECHI KALI :TOTTENHAM VS ARSENAL NANI ATAIBUKA MBABE LEO


Mashabiki wa ligi kuu Uingereza wanausubiri kwa hamu mchezo kati ya Tottenham dhidi ya Arsenal mchezo utakaopigwa dimba la Tottenham Hotspurs Stadium leo hii saa 06:30 jioni.Mchezo huo mkali utaishuhudia Arsenal iliyopo nafasi ya 8 wakitaka kurudi mpaka nafasi ya 5 au 6 ili waweze kucheza Europa UEFA league msimu 2019/20 huku Tottenham wakitaka kurejesha imani kwa mashabiki baada ya kushika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi 

Arsenal wanapointi 50 huku Tottenham wakiwa na pointi 49,kila mmoja anatakiwa ashinde mchezo huo ili walau aingie nafasi 6 bora za juu. Michezo 5 iliyopita baina ya klabu hizo ni Tottenham kushinda michezo 2 sare 2 na alifungwa mchezo mmoja.

Kwa msimu huu klabu hizo zilitoka suruhu ya kufungana mabao 2-2 na mchezo wa leo utaamua nani ni mbabe wa London.Je wewe upo upande gani

Post a Comment

0 Comments