BETI NASI UTAJIRIKE

MECHI KALI LEO: MANCHESTER CITY VS LIVERPOOL JE UPO UPANDE GANI


Klabu ya Liverpool itakaribishwa dimba la Etihad kwa kupigiwa makofi na wachezaji wa Manchester City. Hiyo ni tamaduni kwa ligi mbalimbali  duniani kuipongeza timu iliyotwaa ubingwa kabla ligi kumalizika.

Usiku w leo utakuwa ni mchungu zaidi kwa Guardiola hasa pale anapotakiwa kuwapongeza washindani wake wa ligi ya EPL msimu huu tena wakimuacha kwa pointi 23 kwenye msimamo wa ligi.

Liverpool imecheza michezo 31 ikishinda michezo 28 sare 2 na kufungwa 1 huku ikijikusanyia pointi 86 na imekwisha tangazwa kama ni bingwa wa EPL kwa msimu wa 2019/20. Liverpool imeweka rekodi ya kutangazwa  bingwa kabla ya michezo 21 haijachezwa.

Msimu wa 2018/19 Manchester alitwaa ubingwa wa EPL  akiwa na pointi 98 mbele ya Liverpool aliyekuwa na pointi 97 na kuzifanya timu hizo kuwa na rekodi ya kipekee.

Kama Liverpool atashinda michezo yote 7 iliyobaki basi atafikisha pointi 107 ambazo hazijawahi kufikiwa na klabu yoyote tangu kuanzisha kwa mfumo mpya wa  EPL mwaka 1992. 


Post a Comment

0 Comments