Mshambuliaji wa Barcelona amejikuta akipata wakati mgumu baada ya kucheza mechi 9 na kufunga mabao matatu huku mawili ya penati na moja la kawaida. Huyu si Messi tunayemjua Tangu kutoka Lock Down Barcelona imecheza mechi tisa za La Liga na Messi alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mallorca na alifunga dakika ya 90 kwenye mchezo huo walioibuka na ushindi wa mabao 4-0 Messi alifunga tena kwa mkwaju wa penati kwenye mchezo dhidi ya Leganes walioibuka na ushindi wa mabao 2-0 na bao la tatu alifunga kwenye mchezo wa dhidi ya Atletico Madrid uliomalizika kwa sare ya 2-2 huku Messi akifungwa bao moja kwa penati. Rekodi Mpya Lionel Messi ameweka rekodi ya kuhusuka na mabao 42 ya Barcelona msimu huu akifunga mabao 22 na Assist 20 na kumfanya kufikia rekodi iliyowekwa na Xavi msimu wa 2008/09 alipotengeneza nafasi za mabao 20 Kipi kinamkwamisha Messi baada ya Lock Down Lionel Messi amefikisha umri wa miaka 34 na baada ya miaka kadhaa atastaafu soka,kutofunga kwa mechi 3 mfululizo linaweza kuwa pigo kwa kila mshabiki wa gwiji huyo kwa kudhani kwamba aidha kasi yake imepungua na hataweza kuwa imara tena kama zamani. mkataba mpya anaoutaka Messi ndani ya Barcelona umekuwa mjadala huku klabu hiyo ikionekana kuwa imeshindwa kutimiza kwa nyakati hizi ngumu za kiuchumi. Mbali na kutokuwa na rekodi nzuri kwa msimu huu lakini Lionel Messi anaongoza orodha ya ufungaji mabao akiwa na mabao 22 akifuatiwa na Karim Benzema mwenye mabao 17
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments