BETI NASI UTAJIRIKE

MASHABIKI YANGA WAIPONZA TIMU YAO


Yanga imepigwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa za maji wachezaji wa Namungo walipokuwa wanashangilia baada ya kufunga goli la pili.

 Tukio hilo lilitokea baada ya wachezaji wa Namungo FC kushangilia na kupita karibu na walipokaa mashabiki wa Yanga katika mechi iliyochezwa Juni 23, 2020 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa klabu.


Mchezo huo ulikamilika kwa sare ya kufungana mabao 2-2 ambapo kwa Namungo yalifungwa na Edward Manyama huku yale ya Yanga yakifungwa na David Molinga.

Post a Comment

0 Comments