MANCHESTER UNITED YAKAMATWA PABAYA YASHINDWA KUINGIA TOP 4


Klabu ya Manchester United kwa mara nyingine imejikuta ikishidwa kuingia top 4 baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Southhampton mchezo uliopigwa dimba la Old Trafford 
Southhampton walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Stuart Amstrong dakika ya 12 kipindi cha kwanza lakini Marcus Rashford alisawazisha bao hilo dakika ya 20 na Antey Martial kufunga bao la pili dakika ya 23. Mpaka timu zinakwenda mapumziko Manchester United walikuwa mbele kwa mabao 2-1

Kipindi kilianza kwa kasi lakini kitendo cha kocha Ole Gunnar kuwatoa nje wachezaji muhimu kama Bruno Fernandes,Pogba na Greenwood na nafasi zao kuchukuliwa na Fred ,James na Mctominay nadicho kilichoaribu ushindi wa Manchester United kwan Michael Obafemi akitokea benchi alisawazisha bao dakika ya 90 na ushei na mpira kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Hayo ni matokeo mabovu kwa manchester united kwni wangeshinda mchezo huo wangepanda mpaka nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi na wangekuwa na alama 61 .Sare hiiyo inawafanya Manchester United kusalia nafasi ya tan wakiwa na pointi 59 sawa na Leicester City huku Chelsea wakiwa na pointi 60 nafasi ya 3 

Post a Comment

0 Comments