advertise with us

ADVERTISE HERE

MANCHESTER CITY YAICHAKAZA VIBAYA LIVERPOOL


Klabu ya Liverpool imejikuta ikikubali kipigo cha mabao 4-0 tangu kuanza kwa msimu wa 2019/20. Mpaka klau hiy inatangazwa kuwa bingwa kwa msimu huu walikuwa wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya michezo 31 waliyocheza.

Dakika 25 ya mchezo Kelvin De Bruyne alipachika bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati,Raheem Sterling akifunga bao  la 2 dakika ya 35 huku Phil Foden akifunga bao la tatu dakika ya 45 na kuifanya Manchester City kweda mapumziko wakiwa kifua mbee kwa mabao 3-0.

Dakika ya 66 Alex Chamberlein alijifunga bao na mpaka kipyenga cha mwisho Liverpool alikuwa amefungwa 4-0 

Liverpool imeweka historia ya kipekee msimu huu baada ya kucheza michezo 31 wakishinda michezo 28 wakifungwa 1 na sare 2 na kuwafanya wapate pointi 86 wakiwaacha wapinzani wao Manchester city kwa tofauti ya pointi 23.

Mchezo huo ulikuwa ni muhimu kwa Manchester City kama njia ya kufuta machungu ya kuporwa ubingwa waliotwaa msimu wa 2018/19 lakini pia kupunguza gepu la pointi 23 walizokuwa wameachwa.
Post a Comment

0 Comments