MANARA AFUNGUKA ISHU YA MORRISON KUTUA SIMBA


Klabu ya Simba imesema kuwa haina mpango na mchezaji mahili wa klabu ya Yanga Bernard Morrison ambaye amekuwa akitajwa kuhitajiwa na Simba. inaelezwa kuwa Simba walikuwa wanahitaji huduma ya Morrison ambaye aliwatungua walipokutana Uwanja wa Taifa, Machi 8 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Simba wana wachezaji wengi wazuri na hawana mpango wa kumvuta ndani ya kikosi cha Simba.

"Hakuna, hakuna mpango wa Simba kuzungumza na Morrison, tunatambua kwamba tupo imara na hatuwezi kuzungumza na mchezaji huyo licha ya kwamba yupo vizuri.

"Ninawajua wachezaji wazuri ila hayupo kwenye mipango yetu kwa sasa hayo yanayozungumzwa ni maneno tu hamna kitu kingine," amesema.

Post a Comment

0 Comments