ads

adds

MAKALA:KWA REKODI HIZI ARSENAL ATAVUKA KWELI FAINALI YA FA?



Klabu ya Arsenal inakumbana na Manchester City kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya FA.Arsenal inayonolewa na kocha Mikel Arteta itakuwa na wakati mgumu mbele ya vijana wa Guardiola. 

Msimu huu Arsenal na Manchester City zimekutana mara 2 kwenye michuano ya ligi kuu Uingereza na mara zote Arsenal amefungwa.mchezo  wa raundi ya kwanza Arsenal walifungwa mabao 2-0 na mchezo wa pili walifungwa 3-1

Kwa misimu minne mfululizo Arsenal wamepata ushindi mmoja tu kwenye mechi 10 walizokutana huku wakifungwa 4 na sare 5. Arsenal iliifunga Manchester City mchezo uliopigwa Disemba 21 msimu wa 2015/16

Rekodi za Ligi kuu msimu huu

Arsenal

Msimu huu klabu ya Arsenal imecheza michezo 36 ya EPL ikishinda michezo 13 sare 14 na vipigo 9.huu ni msimu mbovu zaidi kwa Arsenal baada  kujikusanyia point 53 pekee ikiwa nafasi ya 9. mbali na hayo klabu hiyo imekuw na beki dhaifu kwa kuruhusu mabao 45 huku wakifunga mabao 53.Kwa michezo 7 mfululizo Arsenal amepoteza mchezo mmoja dhidi ya Tottenham  huku akipata ushindi dhidi ya Wolves,Liverpool sare na Leicester City

Manchester City

Manchester City msimu huu haikuwa na madhara kulinganisha na msimu wa 2018/19.Imecheza michezo 36 ikipata pointi 75 huku ikikaa nafasi ya 2 msimamo wa EPL.Timu hiyo inasafu imara baada ya kufunga mabao 93 huku wakifungwa mabao 35 tu msimu huu.Wameshinda michezo 24 sare 9 na kufungwa mechi 3. Tangu kurejea kwa EOL mwezi June 22 Manchester City imecheza michezo 9 ikishinda michezo 7 huku ikifunga mabao 27. Manchester City imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Brighton na Newcastle United huku wakiifunga Liverpool mabao 4-0

Swali linabaki ni je Arsenal atavunja mwiko wa Manchester City na kutinga nusu fainali? Tusubiri leo usiku saa 3 na dakika 45

Post a Comment

0 Comments