BETI NASI UTAJIRIKE

MAKALA :TAKWIMU ZA MANCHESTER CITY ZAIPOTEZA LIVERPOOL EPL



Klabu ya Manchester City imeweka rekodi ya kipekee ligi kuu England msimu wa 2019/20.Mbali na kutotwaa ubingwa wa ligi hiyo klabu hiyo imeipoteza klabu ya Liverpool ambao ni mabingwa wa ligi hiyo msimu huu. Manchester City imeongoza kila idara isipokuwa mfungaji bora na ubingwa. Hizi hapa ni rekodi tano za Manchester City msimu huu

1. Idadi ya Mabao

Manchester City imecheza michezo 38 msimu huu na kufunga jumla ya mabao 102 huku ikifungwa mabao 35 tu . Liverpool wao wamefunga mabao 85 huku wakifungwa mabao 33 pekee kwenye mechi 38 walizocheza. Kama utaangalia uwiano basi Manchester City wameongoza mabao 17 mbele ya Liverpool.

Mshindi :Manchester City

2.Idadi ya Pasi 

Manchester City imepiga jumla ya pasi 26,329 msimu huu na kuwafanya waongoze orodha ya upigaji pasi nyingi . Liverpool wanafuatia orodha hiyo wakiwa wamepiga pasi 23,872 .Chelsea wako nafasi ya tatu wakipiga pasi 23,244 na Manchester United wako nafasi ya nne wakipiga pasi 20,059

Mshindi : Manchester City

3. Mechi nyingi bila kuruhusu goli

Manchester City imecheza michezo 38 ila michezo 17 haijaruhusu bao lolote kutikiswa nyavu zao na kuwafanya waongoze orodha hii. Liverpool na Burnley hazijafungwa bao lolote kwa michezo 15 iliyocheza na Leicester City,Manchester United na Shiffield zikicheza michezo 13 bila kuruhusu bao lolote.

Mshindi : Manchester City

4. Upigaji wa Krosi

Manchester City imepiga krosi 914 kwenye michezo 38 waliyocheza wakifuatiwa na Liverpool krosi 896,Shiffield United wakiwa nafasi ya tatu krosi 866 na Chelsea nafasi ya nne kwa krosi 862. 

Mshindi: Manchester City

5. Pasi,Mabao na Ulinzi 

Kelvin De Bruyne ameongoza orodha ya watengenezaji mabao akitengeneza mabao 20 msimu huu ndani ya kikosi cha Manchester city na kumfanya aongoze orodha ya watengenezaji bora wa mabao kwa EPL msimu huu. 

Mshindi : Manchester City

Kipa Ederson Santana de Moraes ndiye anayeongoza kwa kutofugwa bao lolote kwenye michezo 16 aliyocheza msimu huu na nafasi ya pili inashikiliwa na Nick Pope mechi 15 huku David De Gea ,Rui patricio, Allison ,Kespar Scmeichel na Dean Hernderson wakicheza mechi 13 bila kuruhusu bao lolote

Mshindi: Manchester City

Virgil Van Dijk anaongoza orodha ya wachezaji waliopiga pasi nyingi mimu wa 2019/20 akifanya hivyo mara 3,259 nafasi ya pili inashikiliwa na Rodrigo kutoka manchester City akifanya hivyo mara 2,579 nafasi ya tatu ni Harry Maguire akifanya hivyo mara 2519.

Mshindi : Liverpool

Jamie Vardy anaongoza orodha ya mabao akifunga mabao 23 msimu huu na kumfanya atwae kiatu cha ufungaji bora huku akiwafunika Dan Ings na Aubemayang wenye mabao 22 kila mmoja . 

Mshindi : Leicester City



Post a Comment

0 Comments