BETI NASI UTAJIRIKE

MAKALA: NI WAKATI SAHIHI WA MORRISON KUONDOSHWA YANGA


Kwa mara nyingine tena mshambuliaji machachali wa Yanga ameonyesha kiburi na utovu wa nidhamu hadharani baada ya kuondoka uwanjani kabla mechi dhidi ya Simba haijamalizika.Morrison alifanyiwa mabadiliko  dakika 64 ya mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Patrick Sibomana.

Mara baada ya kutolewa uwanjani Morrison hakukaa benchi alielekea moja kwa moja chumba cha kubadili nguo na kubeba vitu vyake kisha kuondoka zake.Haijulikani ni kipi kilisababisha mchezaji huyo kuondoka bila taarifa maalumu lakini kuna uwezekano kukawa hakuna maelewano baina ya uongozi wa Yanga na mchezaji huyo. 

Itakumbukwa wiki kadhaa mchezaji huyo aliingia mvutano na uongozi wa klabu hiyo lakini baadaye mambo yaliwekwa sawa na kufikia hatua ya kumsafirisha peke yake mpaka Kagera kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliomalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0 na mfungaji akiwa ni Morrison.

Binafsi naona ni wakati sahihi kwa klabu ya Yanga kumruhusu mchezaji huyo kuondoka maana amekuwa akiwasumbua mara kwa mara na kuibua migogoro ndani ya klabu hiyo. Kocha Eymael anaonekana kumuhitaji mchezaji huyo lakini binafsi noa ni wakati sahihi kwa mchezaji huyo kuondoshwa la sivyo atatengeneza makundi ndani ya klabu ya Yanga na hatimae washindwe kufanya vyema hapo baadaye.

Post a Comment

0 Comments