BETI NASI UTAJIRIKE

MAJINA YA WARITHI WA MKWASA NA EYMAEL YATAJWA YANGA


Baada ya Yanga kuachana na Luc Eymael ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo wanapiga hesabu za kuwavutia kasi makocha wenye uzoefu na Ligi Kuu Bara ambao ni Patrick Aussems na Hitimana Thiery.

Habari zinaeleza kuwa kuna majina zaidi ya 18 ambayo yametua mezani kwa Yanga kuomba kazi ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa kihistoria.

"Tayari Yanga imeanza mchakato wa kumleta kocha mpya ambaye atafanya kazi ya kukinoa kikosi kwa ajili ya msimu ujao na miongoni mwa wale ambao wanahitajika ni pamoja na Aussems na Thiery wa Namungo.

"Thiery amekuwa bora kwani amemaliza ligi akiwa ndani ya tano bora na aliweza kuwasumbua Yanga hata Simba walipokutana ndani ya uwanja, hivyo anaweza kutua pale, Aussems pia anatajwa kuingia kwenye dili hilo kwani ana uwezo mkubwa na anaitambua Yanga na ligi ya Bongo" ilieleza taarifa hiyo.

Thiery amesema kuwa kwa sasa yupo na Namungo hivyo msimu ukiisha atajua mambo yatakuaje. 

Kaimu Katibu wa Yanga, Simon Patrick amesema kuwa kwa sasa wanaendelea na mchakato wa kumtafuta kocha mambo yakiwa sawa wataweka kila kitu wazi.

Post a Comment

0 Comments