kikosi cha Simba kimewasili salama jijini Tanga tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union utakaopigwa siku ya Alhamisi kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani saa 10 jioni.
Kikosi hicho kitaingia kwenye mchezo huo kikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Alliance kililioupata siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.
Kikosi leo asubuhi kitafanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Mkwakwani ili kujiweka sawa kabla ya mtanange huo ambao unatarajia utakuwa mkali na wakuvutia.
Wachezaji simba wakipokewa na mashabiki
0 Comments