Kwa mara nyingine tena Lionel Messi ameweka rekodi ya kufikisha goli la 700 tangu aanze soka la kulipwa. Messi anakuwa mchezaji wa pili kwa karne ya 21 kuweza kufikisha rekodi hiyo huku nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo akiongoza kwa mabao 728. Messi amefikisha bao la 700 kwenye mchezo wa La Liga dhidi ya Atletico Madrid akiwa na umri wa miaka 33. mpaka sasa mchezaji huyo amecheza michezo 863 na kufunga mabao 700 kwenye michuano yote aliyoshiriki akiwa Barcelona na Argentina. Lionel Messi amekuwa na msimu mzuri kwa kuongoza mbio za kiatu ch dhahabu kwa kufunga mabao 22 la liga huku pia akiongoza kwa kutengeneza nafasi 17 za mabao.
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments