Klabu ya Leicester City imepatwa na pigo baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Bournemouth mchezo wa ligi kuu Uingereza. Jermie Verdie alikuwa wa kwanza kufunga bao la kwanza dakika 23 ya mchezo huo lakini Junior Stanslas alisawazisha bao hilo dakika ya 66 ya mchezo kwa mkwaju wa penati. Dominic Solanke aifunga bao la pili dakika ya 67 huku John Evans akijifunga bao la 3 dakika ya 83 na Dominic Solanke kufunga tena bao la 2 dakika ya 87 ya mchezo huo mkali. Mpaka mpira unamalizika Bournemouth 4-1 Leicester City. Leicester City wanabaki nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 59 baada ya michezo 35 huku Bournemouth wakibaki nafasi ya 18 wakiwa na piointi 30 kwenye michezo 35 waliyocheza
0 Comments