advertise with us

ADVERTISE HERE

LA LIGA: ATLETICO MADRID WAIBANA MBAVU BARCELONA


Klabu ya Barcelona imelazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Atletico Madrid kwenye mchezo wa ligi kuu Hispania La Liga. Mchezo huo mkali uliopigwa dimba la Nou Camp ulishuhudia penati 3 ziipigwa kwa pande zote mbili.

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa alijifunga bao dakika ya 11 lakini Saul Niguez alisawazisha dakika ya 19 .Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilitoka sare ya mabao 1-1.

Dakika ya 50 Lionel Messi alifunga bao lake la 700 kwa mkwaju wa Penati lakini bao hilo lilisawazishwa na Saul Niguez kwa mkwaju wa penati dakika ya 62. Mbali na Barcelona kuutawala mchezo lakini waliondoka na pointi moja pekee.

Matokeo yanaifanya Barcelona kufikisha pointi 70 nyuma ya Real Madrid wenye pointi 71 na mchezo mmoja hapo kesho. Atletico Madrid wamefikisha pointi 59 nafasi ya 3 dhidi ya 57 za Sevilla akiwa nafasi ya 4 .

Kikosi cha Barcelona kilianza na 

Ter Stegen,Semedo,Pique,Lenglet,Alba,Rakitic,Bosquet,Puig,Vidal,Suarez,Messi

Atletico walianza na 

Oblak,Lodi,Felipe,Gimenez,Arias ,Lorente,Tomas,Ferreira,Costa,Correa

Post a Comment

0 Comments