advertise with us

ADVERTISE HERE

KWELI SIMBA LALA LAO YAIBOMOA YANGA MABAO 4-1


Klabu ya Simba SC kwa mara nyingine mimu huu imeonyesha ubora wa hali ya juu baada ya kuwatandika watani zake wa jadi Yanga mabao 4-1 mchezo wa nusu fainali Azam Federation Cup. Mchezo  uliopigwa dimba la Taifa Dar es salaam na kuhudhuliwa na watazamaji elfu 30 uliibua shangwe kwa mashabiki wa Simba waliofuzu  fainali.

Gerson Fraga alikuwa wa kwanza kuipa Simba bao la kuongoza  dakika ya 21 ya mchezo huo lilifanya Simba imalize kipindi cha kwanza ikiwa mbele kwa bao 1-0 lakini kubwa zaidi ni Yanga kushindwa kupiga shuti lolote kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Clatous Chama aliipa Simba bao la pili dakika ya 50  mchezo huo.Miquisonne alifunga bao la tatu dakika ya 52 ya mchezo na super sub Mzamiru Yassin alifunga bao la 4 dakika ya 88 ya mchezo huo akipokea pasi ya super sub mwenzake Meddie Kagere.

Hiki kinakuwa kipigo kikubwa zaidi kwa Yanga msimu huu kwenye michuano yote waliyoshiriki.


Post a Comment

0 Comments