Klabu ya Manchester United imeendelea kuwa tishio kwa kila timu inayokutana nayo ligi kuu Uingereza. Tangu kurejea kwa ligi hiyo juni mosi imecheza michezo mitano ikiwemo minne ya EPL mmoja wa FA mchezo ambao uliipeleka klabu hiyo nusu fainali . Ndani ya michezo minne ya ligi imefunga mabao 12 ikitoka sare mechi moja na nyingine zote ikishinda Hapo jana kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza timu hiyo ilionyesha umahiri mkubwa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Bournemouth mchezo uliopigwa dimba la Old Trafford. Bournemouth walipata bao la kuongoza dakika ya 16 kupitia Junior Stanislas lakini mshambuliaji anayechipukia Mason Greenwood alisawazisha dakika ya 29. Marcus Rashford alifunga bao la 2 kupitia mkwaju wa penati dakika ya 35 Antonio Martial alishindilia msumali wa tatu dakika ya 45 na mpaka kipindi cha pili kinamalizika Manchester walikuwa mbele kwa mabao 3-1 Kipindi cha pili Bournemouth walishambulia kwa kasi na dakika ya 49 wallipata penati iliyofungwa na Joshua King lakini Mason Greenwood alirudi tena langoni mwa Bournemouth na dakika ya 54 alipachika bao la 4 huku Bruno Fernandez akikamilisha ushindi wa manchester United kwa bao la 5 dakika ya 59 Kwa ushindi huo Manchester United inasalia nafasi ya 5 ikiwa na pointi 55 baada ya michezo 33. Kikosi cha Manchester United kiliundwa na De Gea, Wan Bisaka,Lindelof/Bailly,Maguire,Luke Shaw,Pogba ,Matic/Fred,Rashford ,Greenwood,Bruno na Martial/Ighalo
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments