MWINYI ZAHERA ATOA UTABIRI MECHI YA SIMBA NA YANGA JUMAPILIAliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga mkongomani Mwinyi zahera amefunguka Kuelekea mchezo wa Jumapili kati ya Yanga na Simba hatua ya nusu fainali kombe la FA. Kicha huyo amefunguka na kusema 

"Binafsi naona kwamba Yanga ndio wana nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo wa nusu fainali kwa sababu kiufundi wamekuwa na hamasa kubwa ya kushinda katika mechi dhidi ya Simba, sasa wanachotaka ni kuendeleza pale walipoishia, japokuwa watu wanasema Simba watashinda ila kwangu mimi ni tofauti.

"Unajua ukiachana na wachezaji wa Yanga lakini uongozi wa GSM wanajua kuandaa timu vizuri katika mechi na Simba sasa lazima wahakikishe wanapata matokeo kwa kuwa ndiyo njia pekee ya wao kupata nafasi ya kucheza fainali, ikiwezekana ubingwa wa kwenda kimataifa, hivyo naamini Yanga watashinda bila tatizo mchezo huo,"

Post a Comment

0 Comments